Drunk in Fisi: Picha: Elisa JosephDrunk in Fisi: Picha: Elisa JosephPombe kupita kiasi ni mbaya. Hebu angalia huyu mtu amepoteza fahamu na amelala bila yeye kujitambua katika Uwanja wa Fisi. Sisi tulijua ameshakufa na tulishindwa kumsaidia au kumshika kwa sababu tuliogopa tutashtakiwa baadaye. Kumbe, kesho yake tulisikia kwamba baada ya masaa kadhaa aliamka na kuweza kuondoka mwenyewe. Yeye ni mwuza machungwa sokoni ya Tandale na akishauza anakuja kulewa moja kwa moja. Pombe zinazouzwa kule ni kabunguz, mwamba, chibuko, pingu, dakika tatu, wanzuki ikiwemo na gongo. Haya ni baadhi ya matukio ya Uwanja wa Fisi usiku. Balaa tupu. Naomba hizi pombe zipitiwe na TBS.

Too much alcohol is bad. Just look at this person who sleeps unconscious on Hyena Square. We were sure he was dead and we couldn't help or carry him away since we were afraid that could lead to us being arrested later on. But, alas, the day after we heard that after some hours he had woken up and been able to leave on his own. The man sells oranges at Tandale market, and after he has sold some he comes straight here to get drunk. The kinds of alcohol sold at Hyena Square are kabunguzu, mwamba, chibuku, pingu, dakika tatu (three minutes!), wanzuku and gongo. This is what goes on at Hyena Square at night. Disastruous. I would prefer that the alcohol was traded through TBS.