Q: Nani alikushawishi kutengeneza filamu?

Elisa. Sikushawishiwa. Ilikuwa moja ya lengo langu ili latizo kuiokowa jamii. Filamu ina ukweli. Nina lengo la kutengeneza filam ndefu (kuhusu maisha yangu).

Q: Baba yako alikufukuza kwa mara ya kwanza ukiwa na uri gani?

Elisa. Baba yangu alinikataa tangu nikiwa tumboni. Baadae tena. wakati natembea, sijui nilikuwa na umri gani. Mama aliuguwa kichaa wakati huo.

Q: Unasema unajisikia kama si mwathirika lakini furaha yako hasa ni kukutana na baba yako. Je ulikutana nae?

Elisa.. Baba yangu nilikutana naye (nilimuona) lakini kwa mbali sana. Najihisi kuathirika kisaikologia hata nikipanga kuonana nae nikimuona nabadilisha mawazo. Baba yangu nahisi hataki hata akiniona. Nategemea iko siku tutakutana.

Q. Kwanini usiwe na shauku ya kumtafuta baba yako?

Elisa: Kwanza anaishi na mke ambaye anaonekana kama ni adui yangu. Mara ya mwisho nikiwa na umri wa miaka 9 nilikwenda akanipokea vizuri ,aliahidi kunisomesha hatimaye akanifukuzaza. Babo nina hasira na uchungu.

Q Kwanini humsamehe baba yako?

Elisa; Nitamsamehe.

Q: Kwanini wakati mnafukuzwa hamkwenda kwenye familia kusuluhishwa_

Elisa: Baba Kijijini wanamuogopa na hao ndugu zake pia. Nilienda kwa mjomba nae akatutoroka.

Q: Baba yajo yuko mjini au kijijini.

Elisa: Yuko kijijini.

Q: Uko peke (katika familia)yenu?

Elisa: Tupo na kaka yangu na dada yangu. Wao bado wako kijijini .

Q: Kwanini Ulitoroka Kiwohede hata ukakamatwa na kupigwa na polisi?

Elisa: Utofauti wa mazingira. Kule fisi tunakuwa na uhuru wa kufanya unalolitaka.

Q: Nani alikushauri kwenda Kiwohede?

Elisa: Jamila. (mshauri nasaha Kiwohede)

Q: Sasa Unaishi wapi?

Elisa: Nilikuwa Kiwohede kwa miaka 3,umri wangu umepita wa kukaa huko,nimeruhusiwa na sasa najitegemea. Nimepanga chumba urafiki, Manzese..

Q: Nyumbani kwenu ni wapi?

Elisa: Kijiji cha Ilule, Iringa.

Q: Mama yako yuko hai?

Elisa: Ndio yuko kijini, Ilule , Iringa.

Q: Je mama yako anayajuwa matatizo yote uliyoyapata?

Elisa: Hayajui. Familia yote haijui. Inataka muda ili kuwaelezea wasije wakashtuka wakielewa kuwa nimeathirika.

Q: Nakutakia kila la kheri nasi tutafata mfano wako kwa ujasiri wa kutengeneza film. Je rafiki yako Khadija yukoje?

Elisa; Khadija amepona na amebadilika tofauti na kwenye filamu.

Q: Mazoezi ya Mpira uliendelea nayo kwa muda gani?

Elisa: Bado naendelea nayo. Kwa sababu niko kwenye timu ya mpira wa miguu ya wanawake. Sasa tuko daraja la pili.

Q: Unawashauri nini vijana?

Elisa: Wajue sheria na haki zao. Wakipatwa na matatizo wawe tayari kupokea ushauri na kwenda kwenye mashirika ya ustawi wa jamii. Pia kujilinda wenyewe ili kuepukana na maradhi.

Q: Sasa una umri gani?

Elisa: Nina umri wa miaka 23.

Q: Mwaka gani ulianza maisha ya uwanja wa fisi?

Elisa: Kuanzia mwaka 1997 mpka 2003 nilipo shauriwa na Kiwohede na kuhamia huko.

Q: Katika kipindi chako chote cha maisha ya ukahaba uwanja wa fisi, hukuwahi kupata mimba na kuitoa?

Elisa: Bifsi yangu najiepusha na mambo matatu. 1. Namwogopa Mungu ingawa nilitenda dhambi lakini niliomba msamaha kila nikipata muda 2. Naogopa kuuwa na 3. Sipendi chuki na watu (nafurahi na watu wote).

Q: Je huko Uwanja waFisi , wateja wenu ni walevi tu?

Elisa: Kwa kawaida ni hao wa shilingi nia saba lakini wako wateja wa shililing elfu tano hadi kumi ambao hawataki kutumia kondomu (inawezekana wakawa na virusi).

Q: Yule mama aliekuleta Dar kufanya kazi unaona?

Elisa: Hapana. Yeye alinipeleka kwa mtu mwengine akapewa shilingi elfu kumi na kuondoka.

Q: Yule aliyekununua ulikaa naye kwa muda gani.

Elisa: Miaka mitatu bila ya kunilipa mshahara, nilibakwa na mume wake na nilipodai haki yangu alinipeleka polisi hatima yake niliishia jela.

Q: Utatumia mbinu gani kuwaelimisha akinamama vijijini ili wasiwaruhusu watoto wao kuja mjini kufanya kazi za ndani?

Elisa: Kuwe na utaratibu wa Serikali za vijiji kushirikishwa na kuelewa badala ya kinamama kukubaliana wenyewe tu na kurubuniwa kwa doti ya vitenge na kiasi kidogo cha pesa.

Shukrani;

Shukrani kwa ujasiri juu ya historia na kujitambua nasi tutakuwa na malengo kutokana na mafunzo ya filamu na ushauri tunaoupata kotoka Kiwohede

Hisia;

Filam hii inaleta mabadiliko katika jamii. Ni vizuri watu kupima afya na kupata ushauri kwani inawawezesha kujielewa kama wameathirika wataepuka kusambaza na kama hajaathirika watajilinda. Pia inawaondoshea hofu kuwa jamii itawatenga wakigundulika kuwa wameathirika. Vilevile inawapa hamu na uhuru wale wanaoona vigumu kujiweka wazi. Aidha inaonekana kuwa mazoezi kwa muathirika ni moja ya njia muhimu inayomwezesha kujikinga na vitendo vya ngono na kuepukana na fikra potofu za kumkatisha tama kimaisha.